WAKENYA WALAUMIWA KWA KUCHAPISHA TAARIFA MBAYA MITANDAONI KUHUSIANA NA KIFO CHA MBUNGE WA KASIPUL, ONG’ONDO WERE.

Spika wa Bunge la Kitaifa, Moses Wetang’ula, amekosoa hisia za umma kuhusu mauaji ya Mbunge wa Kasipul Charles Ong’ondo Were, akitaja baadhi ya taarifa zinazo chapishwa mitandaoni kuwa zisizo na moyo wa huruma.

Wetangula amesema kuwa wakenya wengi kwa sasa wamekuwa wenye gadhabu na hata kukosa kutathmini kauli wanazo chapisha mitandaoni kutokana na kisa hicho cha kuhuzunisha.

Akizungumza baada ya viongozi wa bunge la kitaifa kutembelea familia ya marehemu Were, spika huyo wa bunge la kitaifa, ameionya jamii ya marehemu dhidi ya kuzingatia masuala taarifa hizo na badala yake kumuomboleza mpendwa wao kama walivyo mfahamu.

Aidha amewataka viongozi wa bunge la kitaifa kutoa taarifa muhimu zinazo weza kusaidia katika uchunguzi dhidi ya kisa hicho huku akiwasisitiza kuhakikisha kuwa wanaimarisha usalama wao.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *