RAIS WILLIAM RUTO ASEMA WAKENYA WAMEKUMBATIA BIMA MPYA YA SHA.

Zaidi ya wakenya milioni 22 wamejisajili kwenye mpango wa Taifa Care kwenye bima mpya ya afya SHIF tangia kuanzishwa kwa mpango huo mwaka jana.

Ni kauli ya rais William Ruto ambaye amesema angalau wakenya elfu 45 hujisajili kwa SHA kila siku.

Akizungumza katika ikulu ya rais kwenye zoezi la kukabidhi magari wizara ya afya, Rais Amesema kuwa hatua hiyo inadhihirisha kuwa wakenya wamenza kukumbatia mpango huo mpya wa afya.

Waziri wa afya Aden Duale ameelezea kupata uungwa mkono mkubwa zaidi kutoka kwa baraza la magavana katika kufanikisha majukumu yake kwa taifa.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *