Idara ya polisi nchini imeahidi kuwekaza jitihada zaidi katika suala la kuwahakikishia wananchi wa kaunti ya Tana River usalama wao.
Kulingana na inspekta wa polisi nchini Douglas Kanja, idara hiyo itatoa fedha za kuwapa mafunzo maafisa wapolisi katika kitengo cha NPR, ambao watashika doria katika eneo hilo.
Akizungumza katika ziara yake kule kaunti ya Tana River, amewahakikishia maafisa wa usalama kaunti hiyo, kutatuliwa kwa changamoto ya ukosefu wa nyumba katika kambi zao Tana River.
Kwa upande wake seneta wa kaunti ya Tana River, Danson Buya Mungatana amewataka maafisa wa polisi, kuongezwa katika eneo hilo ili kudhibiti mizozo ya mara kwa mara, ambayo hushuhudiwa katika mpaka wa kaunti hiyo na Kitui, sawa na Garissa.