WAHADHIRI WA VYUO VIKUU NCHINI WAMKOSOA WAZIRI WA ELIMU EZEKIEL MACHOGU

Wahadhiri wa vyuo vikuu nchini wamemkosoa waziri wa elimu Ezekiel Machogu kufuatia tangazo lake kuwa serikali haitafadhili tena vyuo vikuu vya umma.
Katibu mkuu wa chama cha wahadhiri-UASU- Constantine Wasonga, amesema pendekezo hilo halina msingi wowote na litaathiri pakubwa shughuli vyuoni.
Wasonga amesema kuwa hakuwa na imani na uteuzi wa Machogu katika wizara ya elimu na dukuduku yao imedhihirika sasa wakiapa kuwa kamwe hawatakubaliana na uamuzi wa waziri hiyo.
Aidha wametishia kuwa wana uwezo wakianzisha mchakato kwa rais William Ruto kuhakikisha kuwa Machogu anaondolewa kwenye wizara hiyo.