Ongezeko la uhalifu unaotekelezwa na vijana kaunti ya mombasa umechochea mkutano kati ya maafisa wa usalama, viongozi na wahudumu wa bodaboda kutoka mitaa ya kisauni na mtopanga. Mkutano huo umeafikia kuwa wahalifu na wazazi wao wakamatwe ili kuleta uwajibikaji na kukomesha uhalifu.
Mbunge wa Kisauni Rashid Bedzimba amesisitiza haja ya wazazi hao kuchukuliwa hatua kwani wengi wao ndio wanaosababisha hali ya usalama inadorora kutokana na kile alichokitaja kuwa wanawaficha wana wao wahalifu majumbani.
Wadau hao wa usalama wamesema kuwa hali ya utovu wa usalama inayosababishwa na vijana wenye umri mdogo inapelekea kudorora kwa shughuli za biashara katika eneo bunge hilo la Kisauni.
Aidha wapendekeza idara ya usalama kuwakamata wale wanaosafirisha na kununua mali ya wizi kutoka kwa vijana hao huku wakiamini kuwa ushirikiano baina yao na idara ya usalama itasaidia kudhibiti hali hiyo ya utovu wa usalama.
VISA VYA UHALIFU VINAENDELEA KUSHUHUDIWA KISAUNI

