Viongozi wa kaunti ya Meru wamesisitizwa kudumisha umoja kati yao na kuhakikisha kuwa jamii za eneo hilo zinaishi kwa amani.
Ni wito ambao umetolewa na rais William Ruto, katika kikao na viongozi wa kisiasa eneo hilo, ambapo amewasisitiza kusaidiana katika kuwaleta wananchi wa eneo hilo pamoja.
Rais Ruto amesema kuwa hatua yao, kudumisha umoja itawasaidia katika kubioresha shughuli za maendeleo ya jamii na kaunti ya Meru kwa jumla.
Viongozi hao aidha wameonywa dhidi ya kuendeleza tofauti zao za kisiasa na badala yake kuungana mkono, hadi msimu wa kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2027 zitakapo wadia.
Haya yanajiri baada ya aliyekuwa gavana kaunti ya Meru, Kawira Mwangaza kubanduliwa mamlakani na wawakilishi wadi na wadhifa wake kuchukuliwa na Isaac Mutuma.