SERIKALI YA KITAIFA YATAKIWA KUTATAUA CHANGAMOTO ZA WANANCHI KAUNTI YA TANA RIVER.

Wito umetolewa kwa viongozi wa kitaifa kushirikiana na wale walioko katika kaunti ya Tana River ili kutatua changamoto za kiusalama eneo hilo.

Wakiongozwa na gavana wa kaunti hiyo Dhadho Godana wamesema kuwa kuna haja ya serikali kutatua vita vya mara kwa mara katika kaunti hiyo.

Gavana huyo amelalamikua suala la wananchi kuwawa na rasilimali zao kuharibiwa kila uchao wakati kunapo shuhudiwa mizozo hiyo.

Aidha pia amewataka wananchi kushirikiana na viongozi wa kisiasa katika kutatua changamoto za kaunti hiyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *