Kenya imepiga hatua kubwa zaidi katika kukabiliana na maradhi ya malaria katika maeneo tofauti ya taifa hili.
Haya ni kulingana na katibu wa huduma za afya nchini daktari Mary Muthoni, ambaye amesema, kwa kutumia mfumo wa kidijitali, takriban wakenya milioni 28 katika kaunti 24 za taifa hili walinufaika na neti zilizotibiwa.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari, katibu Muthoni amesema kuwa idadi hiyo, ni sawa na asilimia 94, hatua ambayo inadhihirisha jinsi ambavyo taifa, limejitolea kuwalinda wananchi wake dhidi ya ugonjwa huo.
Kwa upande wake mkurugenzi wa afya katika kaunti ya Kilifi, daktari Hassan Leli, amesema kuwa watatumia vijana katika kuendeleza hamasa kwa wananchi kujilinda dhidi ya maradhi ya Malaria.

