KAMATI YA MISWADA KATIKA BUNGE LA SENETI YAFANYA KIKAO NA WAWAKILISHI WADI KWENYE BUNGE LA KAUNTI YA KILIFI.

Kamati ya sheria andalizi ikiongonzwa na mwenyekiti wake ambaye ni  seneta wa Tharaka Nithi Sen. Mwenda Gataya, imepongeza bunge la kaunti ya Kilifi kwa kufuata sheriza muhumu za utoazaji kodi wananchi wa kaunti ya kilifi.

Akizungumza baada ya kufanya kikao na wawakilishi wadi kwenye bunge hilo, mwenyekiti huyo amesisitiza haja ya hamasa zaidi kwa viongozi wa bunge hilo ili kuboresha utendakazi wao.

Gataya amesema kuwa wameweka miadi ya kufanya vikao vya kuwapatia mafunzo zaidi kuhusiana na utunzi wa sheria.

Ni hatua ambayo imepongezwa na spika wa bunge la kaunti ya Kilifi Teddy Mwambire ambaye amependekeza kufanyika kwa vikao vingi zaidi sawia na hivyo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *