MBUNGE WA ENEO LA KASIPUL KAUNTI YA HOMA BAY ONG’ONDO WERE AAGA DUNIA BAADA YA KUPIGWA RISASI.

Wizara ya usalama nchini imewahakikishia wakenya kuwa itafanikisha uchunguzi dhidi ya kifo cha mbunge wa Kasipul, kaunti ya Homa Baya Charles Ong’ondo Were.

Bunge Ong’ondo Were aliaga dunia jana saa moja unusu usiku, baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana, wakiwa juu ya pikipiki, katika mzunguko uliokaribu na makafani ya City Motuary kaunti ya Nairobi, alipokuwa akienda nyumbani baada ya kudhuria kikao cha bunge.

Akizungumza na waadishi wa habari katibu katika wizara ya usalama nchini Raymond Omollo, amesema kuwa tayari amefanya mazungumzo na wakuu wa idara ya usalama nchini na wameanzisha uchunguzi dhidi ya kifo chake.

Baadhi ya viongozi wa ODM katika bunge la kitaifa, wamejitokeza kuomboleza kifo cha mbunge huyo, wakiongozwa na kiongozi wa wachache katika bunge la kitaifa, Mohammed Junet pamoja na mwakilishi wa kike kaunti ya Homa Baya, Joyce Atieno Bensuda, wameitaka idara ya usalama kuharakisha uchunguzi dhidi ya kifo chake.

Mbunge huyo Charles Ong’ondo Were, amekumbana na mauti yake takriban miezi miwili, baada yake kudai kuwa maisha yake yako hatarini.