Wito umetolewa kwa vijana wa kaunti ya Taita Taveta kusitisha utumizi wa mihadarati katika maeneo yao mashinani.
Kulingana na gavana wa kaunti hiyo Andrew Mwadime, idadi kubwa ya vijana katika kaunti hiyo wameendelea kuathirika kiafya kutokana na utumizi wa mihadarati kupita kiasi.
Akihutubua umma katika kaunti hiyo Mwadime amewataka kutobugia pombe mwaka huu wa 2025 na badala yake kuangazia masuala ya kupata ajira na kuweka akiba ili fedha hizo ziwasaidie kuanza biashara mwaka ujao.
Mwadime amewataka viongozi wa jamii mashinani kuendelea kuhubiri injili hiyo vijijini ili kuhakikisha kuwa wananusuru maisha ya vijana katika maeneo yao.

