Serikali ya kaunti ya Taita Taveta inapania kuzindua ufadhili wa masomo kwa wanafunzi watakaojiunga na kidato cha kwanza juma lijalo.
Wizara ya elimu chini ya waziri Gloria Monikombo imesema kuwa ufadhili huo utasaidia sana jamii zisizojiweza kwani kuna wengi ambao wanahitaji ufadhili huo ila hawana uwezo wa kifedha
Waziri huyo amesema kwa sasa wanashirikiana na maafisa tawala kutambua wanafunzi ambao wanahitaji msaada huo wa kimasomo
UFADHILI WA MASOMO KWA WANAFUNZI WA KIDATO CHA KWANZA KUANZISHWA WIKI IJAYO

