MPANGO WA SERIKALI KUU KUAFIKIA UPANZI WA MITI BILIONI 15 UKAKOSA KUAFIKIWA

Huenda mpango wa serikali kuu kuafikia upanzi wa miti bilioni 15 kufikia mwaka wa 2032 ukakosa kufaulu, kutokana na hatua ya baadhi ya miti hiyo kupandwa katika maeneo kame ambapo miti hiyo hushindwa kustahimili kiangazi kikali.
Haya ni kwa mujibu wa mwanaharakati wa kimazingira katika shirika KILIFI CLIMATE CHANGE GOVERNANCE PLATTFORM, Kelly Robert Banda akiwa   katika eneo la Kidundu mjini kilifi kaunti hii ya Kilifi na kuishauri serikali kuu kuangazia upanzi wa miti ya mikoko, iwapo inahitaji kuafikia malengo yake, ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Kauli yake imeungwa mkono na Francis Thoya mmoja wa wanaharakati hao ambaye amesema kuwa upo umuhimu wa kuwepo kwa mikakati ya kutathmini ukuaji wa miti inayopandwa kila wakati huku Dan Gona akisema kuwa tayari wamechukua hatua ya kuhamasisha vijana nyanjani, kutekeleza suala hilo.
Aidha, baadhi ya akina mama wanaojihusisha na masuala ya upanzi wa miti ya mikoko katika eneo hilo la Kidundu wakiongozwa na Dama Karisa pamoja na Sidi Karisa, wameeleza kunufaika pakubwa na miti ya mikoko katika eneo hilo.