TETESI ZA UHAMISHO ULAYA, JUMANNE

Klabu ya Manchester United imekamilisha usajili wa shabaha yao nambari moja katika dirisha la usajili majira haya ya kiangazi.

Mashetani Hao wekundu wamemnasa Manuel Urgate kutoka Paris S Germain.

Dau la Euro million 60 limehusika kwenye uhamisho huo, na mchezaji huyo raia wa Uruguay anatarajiwa kusafiri hii leo hadi jiji la Manchester kufanyiwa vipimo vya kiafya.

🔴Red Devils wanatarajiwa kumwachilia kiungo Scott McTominay kuelekea Napoli kwa Dau la pauni milioni 30.

🔵Mshambuliaji raia wa ubelgiji Romelu Lukaku anatarajiwa kutua Napoli baada ya mchakato wa muda mrefu uliohusisha uhamisho wake kuelekea klabu hiyo

Kulingana na ripoti ni kuwa Sasa kilichosalia ni vyeti kukaguliwa na Lukaku asafiri kwa vipimo vya kiafya huko Napoli.

🟡Cristiano Ronaldo amethibitisha kuwa huenda akastafu soka la kulipwa katika klabu yake ya Sasa Al Nassir.

Amethibitisha kuwa huenda akaachana na soka ndani ya kipindi cha miaka 2 au mitatu ijayo.

🔴Huenda fowadi wa Italia Federico Chiesa huenda akaibukia uingereza na kujiunga na klabu ya Liverpool.

Katika ripoti za hivi punde zaidi Chiesa ameripotia kuwa Kati ya wachezaji ambao huenda wakasajiliwa.

Klabu yake ya Juventus imetangaza kuwa haina mpangoo na Mshambuliaji huyo msimu huu na huenda akabaki bila klabu dirisha la uhamisho kilifungwa

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *