Zaidi ya wasichana 100 katika kaunti ya Kilifi walihisika katika michuano ya kinadada ya ukumbusho wa Shujaa wa wamijikenda Mekatilili wa menza katika eneo bunge la Magarini wikendi ilopita.
Hii imetafsiriwa kama mwamko mpya katika soka la kinadada katika ugatuzi hilo ambalo soka la wanaume limeshamiri kuliko la kinadada.
Hata hivyo kulingana na waandalizi wa mashindano hayo ni kuwa bado soka la kinadada linapitia changamoto chungu nzima. Elizabeth Hinzano ambaye ni naibu mwenye kiti wa Kilifi Soccer Forum ni kuwa ukata wa kifedha ndio jambo linalofelisha akinadada wa Kilifi.
Kwa upande wake Emily Tatu ambaye ni nahodha wa mabingwa Kilifi Starlets kwenye makala ya pili anasema mashindano hayo yamewapa fursa kinadada kuonesha talanta zao uwanjani.

