Waziri wa mazingira na misitu nchini Soipan Tuya amesema kuwa wanapania kuanzisha mikakati ya kuweka sheria ya kuhakikisha uuzaji wa hewa kaa (CARBON CREDIT) kwa mataifa ya nje inawanufaisha zaidi watunzaji wa mazingira zaidi nchini Kenya.
Akizungumza kwenye kijiji cha Makongeni na Gazi eneo bunge la Msambweni kaunti ya Kwale Tuya amesema kwa sasa hakuna sheria mwafaka ambayo inahusiana na utunzaji wa mikoko na uuzaji wa hewa kaa ambayo ni biashara inayopaswa kuwanufaisha wananchi.
Tuya amesema watahakikisha pia wanapana kupania mradi na pia kujaribu kwenye maeneo mengine kanda ya pwani ili kuwafaidi wakazi.
Naye gavana wa kaunti hiyo Fatuma Achani ameutaja mradi huo kuwa wenye manufaa mengi kwa wenyeji kwani kumekuwa na mataifa ya kigeni ambayo yamekuwa yakizuru eneo la Gazi ili kujifunza mbinu hiyo ambayo imekuwa ikisaidia kutunza mazingira.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na mbunge wa Msambweni Faisual Bader ambaye pia amesema kuna haja ya mradi huo kuimarishwa ili kuzidi kuwafaidi wenyeji.
SOIPAN TUYA ASEMA WANAPANIA KUANZISHA MIKAKATI YA KUWEKA SHERIA YA KUIMARISHA UUZAJI WA HEWA KAA KIMATAIFA

