Mbunge wa Voi kaunti ya Taita Taveta Abdi Chome watawasilisha malalamishi yao kwa serikali ya Uingereza kuhusu kupata fidia kutokana na athari ya vita ya kwanza ya dunia.
Kwa mujibu wa Mbunge huyo vita hiyo iliathiri pakubwa kuongezeka kwa jamii ya Wataita na Wataveta na pia kuathiri shughuli za kilimo kwa asilimia kubwa.
Kauli yake inajiri huku maadhimisho ya vita ya kwanza ya dunia iliyofanyika kati ya mwaka wa 1914 na 1918 ikianza katika kaunti hiyo ya Taita Taveta.
ABDI CHOME ATISHIA KUWASILISHA MALALAMISHI KWA SERIKALI YA UINGEREZA

