SERIKALI YA KITAIFA YA WEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA MARADHI YA HEPATITIS.

Asilimia tatu ya Wakenya wanaugua ugonjwa wa ini, unaojulikana kwa kimombo Hepatitis B na C.

Ukosefu wa ufahamu kuhusu ugonjwa huo, hasa katika maeneo ya mashinani, umetajwa kuwa changamoto kuu inayokwamisha juhudi za kukabiliana msambao wa maradhi hayo.

Akizungumza na wanahabari jijini, Mombasa wakati wa hafla ya kuadhimisha Siku ya Hepatitis Duniani, Mkurugenzi Mkuu wa Afya, Dkt. Patrick Amoth, amesema kuwa Serikali ya Kitaifa, imeweka mikakati mbalimbali ya kupambana na ugonjwa huo, ikiwemo kuhamasisha jamii ili kujitokeza kufanyiwa vipimo.

Dkt. Amoth, amesema kuwa serikali inagharamikiaa dawa, za wagonjwa wa Hepatitis na watapokea matibabu bila malipo, hatua inayolenga kuimarisha juhudi za kudhibiti ugonjwa huo.

Wakati huo huo, Dkt. Amoth ameongeza kuwa kufikia sasa, watu mia tatu kote nchini, wamethibitishwa kuugua ugonjwa wa Mpox, ambapo kaunti ya Mombasa imeripoti visa 139 na watu watano kufariki kutokana na ugonjwa huo.

Dkt. Amoth ameeleza kuwa Wizara ya Afya, inashirikiana kwa karibu na Serikali ya Kaunti ya Mombasa, katika juhudi za kudhibiti ugonjwa wa Mpox, ikiwemo kuhamasisha jamii, kuongeza shughuli za vipimo dhidi ya ugonjwa huo, pamoja na kufuatilia kwa karibu wagonjwa waliothibitishwa kuugua MPOX, ili kuhakikisha wanapokea huduma inayofaa na kuzuia ueneaji zaidi wa ugonjwa huo.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *