Rais William Ruto ameendelea kuwapatia ahadi kemkem wachezaji wa timu ya Harembe Stars, iwapo watafaulu kushinda mechi zilizoko kwenye madaraja tofauti katika mshindano ya CHAN.
Akizungumza na wachezaji hao hii leo, rais Ruto ameahidi kuwazawadi shilingi milioni moja kila mchezaji na nyumba za vyumba viwili vya malazi, kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba za bei nafuu, iwapo watashida robo faninali ya michezi hiyo na nyumba yenye vyumba vitatu vya malazi kila mmoja, iwapo watashinda mchuono wa semi fainali.
Ikumbukwe kwamba wakenya wamekuwa wakitozwa ushuru kwenye mishahara yao ili kufanikisha mpango wa ujenzi wa nyumba hizo.
Aidha, amewapongeza wakenya kwa kuendelea kuunga mkono timu ya taifa ya Harembe Stars, katika michezo hiyo ya Chan inayo endelea katika uwanja wa Kasarani kaunti ya Nairobi.

