Mwakilishi wadi ya Ronge kaunti ya Taita Taveta, Dorcus Mlughu amepinga madai yaliyo ibuliwa dhidi yake na naibu spika kwa bunge la kaunti hiyo Anselm Mwadime, kuhusiana na hatua yake kutohudhuria vikao vinane vya bunge hilo.
Kulingana na Mlughu, matamshi hayo sio ya kweli na tayari ameelekea mahakamani ili kupinga uamuzi wake, kubanduliwa katika nafasi ya uwakilishi wa wadi hiyo.
Akizungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza, baada ya tangazo hilo juma lililopita, Dorcas amedai kuwa mwananchi wa wadi yake, ndiye aliye na uwezo wa kumuondoa mamlakani na wala sio spika wa bunge.
Kiongozi huyo anadai kufurushwa kwake bungeni, ni mojawapo ya dhulma dhulma dhidi ya wanawake katika uongozi wa bunge la kaunti hiyo.

