SERIKALI YA KAUNTI YA MOMBASA YA WEKA MIKAKATI YA KUKABILIANA NA MARADHI YA EBOLA.

Idara ya afya kaunti ya Mombasa imewahakikishia wananchi wa kaunti hiyo kuwepo kwa mikakati, ya kukabiliana na maambukizi wa maradhi ya Ebola ambayo yameanza kuripotiwa, katika baadhi ya mataifa ya Afrika Mashariki.

Kulingana na afisa mkuu wa afya kaunti ya Mombasa Pauline Oginga, ni kuwa idara hiyo kwa ushirikiano na mashirika mengine ya kijamii katika kaunti hiyo, yameendelea kufanya vipomo kwa baadhi ya watu, wanaoingi katika taifa hili kupitia mpakani na hata katika uwanja wa ndege wa kaunti hiyo.

Akizungmza na wanahabari afisa huyo amesema kuwa licha ya kuwepo kwa baadhi ya watu ambao, hutumia njia za mkato kuingia humu nchini kutoka taifa jirani la Tanzania, maafisa wa idara hiyo wako ange kuhakikisha kuwa wanakabiliana na yeyote atakae ripotiwa kuugua maradhi hayo.

Wakati uohuo amesema kuwa tayari serikali ya kaunti ya Mombasa, imewapa mafunzo baadhi ya maafisa wa afya, kuhusiana na masuala ya njisi wanavyoweza kukabiliana na visa vya maambuzi ya Ebola.

Amesema kuwa maafisa hao ni wale waliokuwa wakikabiliana na maradhi ya covid19 katika kaunti hiyo.