PROFESA RAPHAEL MUNAVU ATEULIWA KUWA MWENYEKITI WA JOPO LA KUTATHMINI MTAALA WA CBC.

Rais wa taifa hili Dktr William Kipchirchir Arap Samoei Ruto, ameunda jopo la wataalumu wa masuala ya elimu, ili kutathmini utendakazi wa mtaala mpya wa umilisi wa CBC na kumteua profesa Raphael Munavu, kuwa mwenyekiti wa jopo hilo.

Jopo kazi hilo litafanya tathmini ya mtaala huo na kusoma sheria zote zinazosimamia sekta ya elimu ya msingi na kutoa mapendekezo ya iwapo upo umuhimu wa kufanyia marekebisho baadhi ya sheria hizo, ili kushughulikia utata unaokumba mtaala huo.

Wakati uohuo jopo hilo pia, limepewa jukumu la kutathmini mfumo wa mitihani na pia kutathmini mfumo wa elimu na mafunzo ya ualimu, kwa wanafunzi wa shule ya awali.

Aidha, rais pia ameagiza chama cha wafanyikazi kuangazia sera za kuajiri walimu na usimamizi wa shule kwa ujumla.

Mwenyekiti huyo Profesa Munavu, aliwahi kuwa profesa wa Kemia katika Chuo Kikuu cha Nairobi tangu mwaka 1976.

Yeye ni mtaalamu wa Oganic Chemistry, Mazingira na Viwanda.