MASSA HAMISI SALIM ATEULIWA KUWA KAIMU MKURUGENZI WA DCI.

Tume ya huduma za polisi, NPSC imemteua Massa Hamisi Salim kuwa kaimu mkurugenzi wa idara ya upelelezi DCI.

Kupitia mtandao wa twitter tume hiyo imehoji kuwa Salim atashikilia nafasi hiyo hadi pale wadhfa huo utakapojazwa kwa mujibu wa utaratibu wa kisheria.

Hatahivyo tume hiyo imesema kuwa katika muda wa majuma mawili yajayo wadhfa huo utapata mkurugenzi wa kudumu baada ya George Kinoti kujiuzulu.

Tayari idara ya polisi imetangaza kuwa wazi nafasi ya mkurugenzi wa DCI na kuwataka wakenya wanaopania kupata wadhfa huo watume maombi yao kufikia alhamisi ijayo tarehe 6 mwezi Oktoba.