Hotuba ya kwanza ya Rais William Ruto katika bunge la 13 haikukosa vijembe vya kisiasa huku rais akisifia ukomavu wa siasa za Kenya na demokrasia.
Rais Ruto akionekana kumlenga rais Mstaafu Uhuru Kenyatta kwa kusimama na kiongozi wa upinzani wakati huo, licha ya kuwa serikalini.
Rais Ruto sasa amesema kuwa serikali inatafuta mbinu za kuwasaidia Wakenya walio kwenye sekta ya biashara ndogo ndogo kuweka akiba ya uzeeni akisema kuwa mfumo wa sasa wa kuweka akiba kupitia hazina ya nssf hauwezi kumsaidia mtu anapostaafu kazini.
Hayo yakijiri, Rais William Ruto amewaeleza wabunge na maseneta wa bunge la 13 kuhusu mipango aliyo nayo kuhakikisha kuwa anatekeleza ahadi za muungano wa kenya kwanza ambazo zitahitaji kuidhinishwa kuwa sheria. Miongoni mwao ni kuhakikisha mgao zaidi kwa idara ya mahakama na mpango wa hazina ya hasla kutimizwa.

