Zaidi ya watu elfu nane wakiwemo watoto wenye umri wa miaka 10 kaunti ya Mombasa, wanadaiwa kuwa watumizi wa dawa ya kulevya aina ya Heroin.
Takwimu hizo ni kwa mujibu wa Shirika la kukabiliana na dawa za kulevya na pombe haramu nchini NACADA, ambalo limesema kuwa kaunti ya Mombasa ni mojawapo ya kaunti ambazo, zinaongoza katika utumizi wa dawa hiyo ya kulevya.
Akizungumza katika kikao cha kuhamsisha viongozi wa dini ya kiislamu kuhusiana na tatizo hilo, afisa mkuu wa shirika hilo ukanda huu wa Pwani George Karisa, amesema kuwa suala hili lingekabiliwa iwapo jamii ingewahamasisha vijana kuhusiana na athari zake.
Kwa upande wake mmoja wa viongozi wa baraza la SUPKEM kaunti ya Mombasa ustadh Mahamood Abdulahi, amelalamikia hatua ya idadi kubwa ya vijana kuathirika na utumizi wa mugukaa na sigara, licha yake kuathiri afya zao huku akitoa wito kwa serikali, kupiga marufuku bidhaa hizo.

