SERIKALI YA KAUNTI YA MOMBASA INAWEKEZA KUWAWEZESHA VIJANA WANAOZOA TAKA

Naibu gavana wa kaunti ya Mombasa Francis Thoya amesema serikali ya kaunti hiyo itawekeza zaidi katika kuwawezesha vijana ambao wanazoa taka ili wanaufaike.

Kulingana na Thoya kuna makundi mbalimbali ya vijana katika kaunti ya Mombasa ambao wanafanya kazi ya kuzoa taka na makundi hayo yanapaswa kuwezeshwa ili kunufaika kimapato.

Akizungumza huko Shanzu baada ya kukutana na makundi mbalimbali ya vijana ambao wanajihusisha na uzoaji taka, Naibu Gavana huyo wa Mombasa amesema shughuli kama hizo zimesaidia kuwawezesha vijana kujitenga na makundi ya kigaidi na utumizi wa dawa kulevya.

Vilevile, amesema watawekeza zaidi katika kubuni nafasi za ajira kupitia uzoaji huo wa taka.