SERIKALI KUU YATAKIWA KUHIFADHI ARDHI ZOTE ZENYE UTATA KAUNTI YA LAMU

Wanaharakati wa maswala ya kijamii kaunti ya Lamu wameitaka serikali ya kitaifa kuhifadhi ardhi zote zinazokumbwa na utata wa umiliki katika kaunti hiyo.
Wakiongozwa na Abdulwahid Mohamed, wanaharakati hao wamesema kuwa sehemu kubwa ya ardhi katika wadi ya Mkunumbi imegubikwa na kesi zilizowasilishwa mahakamani.
Kufuatia hilo, Abdulwahid ameshinikiza serikali kutoa uhifadhi wa ardhi zote zenye kesi hadi pale utata huo utakapokamilika.
Kwa upande wake kiongozi wa vijana katika wadi ya Mkunumbi amewaelekezea kidole cha lawama wanasiasa kwa kile alichosema kuwa wamekuwa wakichangia mizozo ya umiliki wa ardhi kutokana na kutoa ahadi wasizozitimiza.