Asilimia kubwa ya vijana kaunti ya Taita Taveta hukosa kujiunga na vyuo vikuu na vyuo kiufundi baada ya kukamilisha kidato cha nne.
Haya ni kwa mujibu wa naibu gavana kaunti hiyo Christine Kilalo ambaye amesema kuwa idadi hiyo kubwa hushindwa kujiendeleza kimasomo kufuatia ukosefu wa karo.
Kilalo sasa amewashauri vijana hao waliomaliza kidato cha nne kujisajili ili kupata mikopo na ufadhili mbalimbali wa kielimu ikiwemo HELB ili waweze kuendelea na masomo yao.
Naibu gavana huyo pia amehoji kwamba kaunti ya Taita Taveta imewekeza pakubwa katika vyuo vya kiufundi akiwashinikiza vijana kujiunga na taasisi hizo ili wajiimarishe kiujuzi.
Kilalo amesema kuwa taasisi hizo zinasaidia sana vijana kuweza kujiajiri wanapomaliza masomo yao badala ya kutegemea kuajiriwa.
IDADI KUBWA YA VIJANA KAUNTI YA TAITA TAVETA HUSHINDWA KUJIUNGA NA VYUO VYA KIUFUNDI

