Seneta mteule kaunti ya Mombasa Miraj Abdillahi ametoa wito kwa wenyeji wa kaunti hiyo kupanda miti kwa wingi ili kulinda mazingira pamoja na kuzuia kushuhudiwa kwa hali ya ukame miaka ijayo.
Miraj amesema mpango huo ambao ulianzishwa na rais William Samoei Ruto unapaswa kuungwa mkono na kuendelezwa ili kudhibiti taifa hili dhidi ya kukabiliwa na ukame unaochangiwa na mabadiliko ya hali ya anga.
Kauli ya Miraj Abdillahi imeungwa mkono na kamishna wa kaunti ya Mombasa John Otieno ambaye amesema itakuwa vyema iwapo kila mwenyeji wa kaunti hiyo atawajibika katika kutunza mazingira kupitia upanzi wa miti.
SENETA MTEULE KAUNTI YA MOMBASA AWAHIMIZA WENYEJI KUPANDA MITI KWA WINGI

