NAIBU KAMISHNA WA ENEO BUNGE LA MAGARINI AWAONYWA WANAOPANIA KUJIHUSISHA NA VISA VYA UDANGANYIFU WA MITIHANI YA KITAIFA

Naibu kamishna wa Magarini kaunti ya Kilifi Peter Thiong’o amewaonya wale ambao wanapania kujihusisha na visa vya udanganyifu kwenye mtihani wa kitaifa wa Gredi ya 6 na darasa la 8 ambao umeang’oa nanga leo Jumatatu.
Kwa mujibu wa Thiong’o mikakati thabiti imewekwa na asasi za usalama kuhakikisha hakuna visa vya udanganyifu ambavyo vinashuhudiwa wakati wa kuandaliwa kwa mitihani hiyo.
Amewataka watahiniwa wa mtihani huo kutia bidii na kusema watakaopatikana wakijihusisha na visa vya udanganyifu watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.