Mbunge wa Lamu Mashariki kaunti ya Lamu Ruweida Obo amesema katika uongozi wake hatambagua mwenyeji yeyote.
Katika ahadi zake amesema atahakikisha jamii ya Awer ambayo inaishi kwenye msitu wa Boni inanufaika kielimu.
Amesema ili jamii hiyo iweze kinufaika na elimu, atahakikisha watoto wa jamii hiyo ambao wanasomea shule ya msingi ya bweni ya Arid Zone hawangaishwi kutokana na ukosefu wa karo.
Ni kauli ambayo imeungwa mkono na naibu Gavana wa kaunti ya Lamu Raphael Munyua na kuwasisitizia wazazi wa jamii hiyo na kaunti ya Lamu kwa Jumla kuhakikisha inawapeleka watoto wao shuleni kwani ni haki yao kikatiba.
RUWEIDA OBO ASEMA JAMII YA AWER INAYOISHI KWA KWENYE MSITU WA BONI ITAIMARISHWA KIELIMU

