RIGATHI GACHAGWA ATARAJIWA KUZINDUA CHAMA CHAKE WIKI HII.

Aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa amesema kuwa atazindua chama chake cha kisiasa wiki hii.

Kulingana na Gachagwa chama hicho atakacho tumia kufanikisha agenda yake ya kuwania uras wa taifa hili mwaka 2027.

Gachagwa amepinga madai ya kushuhudiwa kwa mgawanyiko katika mrengo wa upinzani huku akiwasisitiza vijana kuhakikisha kuwa wanasajiliwa kuwa wapinga kura.

Haya yanajiri wakati ambapo Gachagwa ametoafautiana na kinara wa Wiper Kalonzo Musyoka kuhusiana na uteuzi wa makamishna wa IEBC uliofanywa na rais William Ruto wiki iliyopita.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *