Kinara wa chama cha Wiper, Kalonzo Musyoka amemtaka naibu wa rais Profesa Kithure Kindiki kujiuzulu baada ya mahakama kusema kuwa uteuzi wake ulikiuka sheria za taifa hili.
Kulingana na Kalonzo muungano huo wa upinzani kwa sasa hautambui uwepo kwa naibu wa rais katika taifa hili.
Kalonzo katika kikao na waandishi wa habari, amesema kuwa hatua ya kumuondoa mamlakani aliyekuwa naibu wa rais Rigathi Gachagwa iliendeshwa kisiasa.
Kiongozi huyo amesema hatua ya bunge kushiriki kikao cha kumbandua Gachagwa ili kuwa kwa na malengo ya kunufaisha baadhi ya watu kisiasa.

