REGRAGUI AWAPA SHAVU ATLAS LIONS LICHA YA KUPOTEZA MECHI YA NUSU FAINALI

Mkufunzi wa timu ya taifa ya Morocco Walid Regragui amewapongeza vijana wake wa Atlas Lions kwa kuonyesha kiwango kizuri katika mechi ya Jumatano licha ya kutandikwa kichapo cha 2-0 na timu ya taifa ya ufaransa, kichapo ambacho kiliwafanya kuachana na azma yao ya kuwinda ubingwa wa dunia.

Regragui amesema kumakinika kwa vijana wake ndio jambo lililowapa manufaa katika mashindano ya kombe la dunia ikizingatiwa kwamba mechi ya Jumatano (14 Disemba 2022) Morocco walimiliki mpira kwa asilimia 51 mchezo ambao walionyesha kumakinika tofauti na mechi za awali.

Kwa sasa Morocco wanasubiri kuvaana na Croatia katika mechi ya kutafuta mshindi wa tatu na wanne mtawalia ila mbali na hayo Morocco imeweka rekodi katika mashindano ya mwaka huu kama timu ya kwanza kutoka barani afrika kufika hatua ya semi fainali.