RAIS WILLIAM RUTO AWAONYA MACHIFU DHIDI YA KUTOSISITIZA MASUALA YA ELIMU MASHINANI.

Maafisa wa usalama mashinani katika eneo bunge la Galole kule kaunti ya Tana River, wametakiwa kuwachukulia hatua kali za kisheria wazazi wa watoto wasioenda shuleni.

Haya ni kulingana na rais William Ruto ambaye ametishia kuwafuta kazi machifu pamoja na manaibu wao, wanaofanyakazi katika maeneo ambayo watoto watapatikana mitaani, wakiwa wamekosa kujiunga na taasisi za elimu.

Akizungumza katika eneo hilo, Rais Ruto amewasisitiza wazazi wa kaunti ya Tana River na Lamu, kuzingatia zaidi masuala ya kuhakikisha kuwa wanao wanapata elimu bora.

Rais Ruto ameongea kuwa serikali inaendelea kujitahidi katika kuajiri walimu zaidi kwenye shule za serikali, ili kuhakikisha kuwa kuna usawa kati ya wanafunzi wote katika taifa hili.