WAMILIKI WA MADUKA YA DAWA WAONYWA DHIDI YA KUUZA DAWA KINYUME CHA SHERIA ZA AFYA.

Mamlaka ya kukabiliana na utumizi wa pombe na mihadarati nchini Kenya NACADA, imethibitisha kuwa baadhi ya wakenya hutumia dawa zinazouzwa kwenye maduka ya dawa, kinyume cha muongozo wa madaktari.

Kulingana na naibu mkurugenzi wa NACADA Ann Mathu, watu wengi hutumia dawa hizo kama mihadarati, jambo ambalo ni kinyume na matumizi yaliyo ratibiwa na wizara ya afya.

Mathu, ameonya wamiliki wa maduka ya dawa dhidi ya kuuza dawa aina hizo, pasi na mteja kuonyesha ithibati aliyopewa na daktari, ili kutumia dawa hizo.

Vile vile Ann amewaonya wadada dhidi ya kutumia kemikali za kubadili rangi ya mwili, kwa kile alichosema dawa hizo, zina athari kubwa kwa afya zao, ikiwemo kuwaweka katika hatari ya kukosa kupata ujauzito.