RAIS WILLIAM RUTO ATUMIA MRADI WA NYUMBA KAUNTI YA NAIROBI KUSUTA WAPINZANI WAKE.

Rais William Ruto amewasuta baadhi ya wapinzani wake kwa kuendeleza semi zinazo kejeli utendakazi wa serikali ya Kenya kwanza.

Kulingana na kiongozi huyo wa taifa, serikali yake itaendeleza mikakati ya kufanikisha ahadi ilizotoa kwa wananchi wa taifa hili katika kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka 2022.

Akizungumza katika eneo la Mkuru Kwa Njenga kaunti ya Nairobi, wakati akipeana rasmi nyumba za bei nafuu kwa wananchi, rais amesisitiza viongozi wengine kujitenga na siasa na badala yake kuboresha maendeleo katika maeneo yao.

Aidha, rais Ruto amesema kuwa serikali ya kitaifa itaendeleza mradi wa ujenzi wa majumba hayo, katika maeneo mbali mbali ya taifa hili na kuhakikisha kuwa inaondoa wakenya mitaa ya mabanda.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *