MSHUKIWA WA MAUAJI YA MBUNGE CHARLES WERE AACHILIWA BAADA YA KUKAMATWA KWA MARA YA PILI.

Afisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka ya Umma (DPP), imefanikiwa kukata rufaa ya kuachiliwa kwa mfanyabiashara Philip Aroko, ambaye ni mmoja wa washukiwa wa mauaji ya mbunge wa Kasipul kaunti ya Homa Bay, Charles Were,.

Aroko, alikamatwa tena baada ya mahakama kuu ya Kibera, kubatilisha hatua ya kumwachilia kwa dhamana.

Aroko, alikamatwa mnamo Jumatatu jioni baada ya kuachiliwa kwa dhamana Ijumaa iliyopita, kusubiri matokeo ya uchunguzi kuhusiana na mauaji ya Charles Were.

Aroko aliachiliwa siku ya Ijumaa kwa dhama ya shilingi 300,000 na Hakimu Mkuu wa Mahakama ya Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta Irene Gichobi.

Hakimu huyo alitoa masharti kadhaa ya kuachiliwa kwa Aroko, ikiwa ni pamoja na sharti la kukabidhi mamlaka, hati yake ya kusafiri, kuripoti kwa afisi za DCI mara mbili kwa wiki na kuhakikisha anapatikana anapohitajika.

Aroko na washukiwa wengine, walikamatwa kwa madai ya kuhusika katika mauaji ya mbunge wa Kasipul marehemu Charles Were.