RAILA ODINGA APENDEKEZA KILA KAUNTI KUWA NA TUME YA IEBC

Kinara wa Azimio la Umoja One Kenya Raila Odinga amependekeza kila kaunti  nchini kuwa na tume yake ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC ambayo itaendeleza shughuli zake kwa uhuru pasipo kuunganika na ile ya kitaifa.
Akizungumza katika uwanja wa Kamukunji kaunti ya Naiobi hapo jana, Raila amesema kuwa hali hiyo itasaidia kuhakikisha kuwa kuna usawa katika shughuli zote zinazotekelezwa na tume huru ya uchaguzi na mipaka nchini IEBC.
Aidha Raila amesisitiza kuwa mrengo wa Azimio la Umoja One Kenya hautamruhusu rais William Ruto kujiandalia tume yake ya uchaguzi akisema ni sharti wanaazimio la umoja wahusishwe katika maamuzi ya uundaji wa tume hiyo ya uchaguzi.
Ni kauli iliyoungwa mkono na kinara mwenza wa Azimio la Umoja One Kenya, Martha Karua ambaye amesema kuwa kuna haja ya azimio kuhusishwa katika maamuzi ya uundwaji wa tume hiyo ya uchaguzi.