Vinara wa Ligi Kuu hapa Nchini Kenya Police, wataanza harakati Zao za Kutetea Taji la FKF cup makala ya Mwaka huu, dhidi ya Superior Hotel Fc Kutoka Naivasha, hii ni baada ya Droo ya michuano hiyo Itakayo Ng’oa nanga wikendi Hii kufanyika hapo jana Usiku.
Wanabenki KCB ambao walipoteza kwenye fainali ya makala yaliyopita, watamenyana na Chemogoch kutoka Kaunti ya Baringo, washindi wa mwaka wa mwaka wa Elfu mbili na tatu kakamega Homeboys wakimenyana na JW Foundation.
Kwa Upande Wao washindi wa mwaka wa elfu mbili kumi na Tisa Bandari, wataanza Harakati Zao Dhidi Ya Rwafa FC kutoka kaunti ya Kwale, Bumbani wakivaana na fortune Sacco, Denmarck wakiekeana miadi na Uzalendo kutoka Kaunti ya Kakamega, Huku Mombasa Stars wakizichapa na Ishiara fc ya Embu Kaunti Ugenini.

