Hali ya kiafya ya nguli wa brazil mwite Pele imeanza tena kuzorota akiwa hospital jijini Sao Paulo Brazil ambako anapata matibabu ya saratani.
Nguli huyo mwenye umri wa miaka 82 amekuwa akiandamwa na magonjwa ya mara kwa mara huku akiwa chini ya uangalizi mkali wa madaktari ambao kwa sasa wanataja kwamba hali yake bado haijakuwa shwari.
Mshindi huyo mara tatu wa kombe la dunia alifanyiwa upasuaji wa tumbo mwaka 2021 kutolewa uvimbe pamoja na hivi juzi zaidi ambapo alirudishwa hospitalini kutokana na maradhi ya mapafu.
Kulingana na uongozi wa hospitali hiyo ya sao Paulo ni kwamba pele atalazimika kusalia hospitalini kipindi hiki cha sherehe za krismasi.

