Aliyekuwa mwaniaji wa wadhifa wa ugavana kaunti ya Taita Taveta Patience Nyange amesisitiza haja ya wanawake na vijana kaunti hiyo kushirikishwa kikamilifu kwenye uongozi wa kaunti hiyo.
Nyange amesema anapania kushirikiana na gavana wa sasa Andrew Mwadime sawia na mashirika mbalimbali yasiokuwa ya kiserikali ili kuhakikisha masuala ya vijana na wanawake yanapewa kipaumbele.
Nyange pia ametoa wito kwa viongozi wa kike kushirikiana vilivyo kwa minajili ya kutatua changamoto zinazokumba wanawake katika jamii.

