KAMISHNA WA KWALE AWAONYA WENYEJI DHIDI YA KUNYAKUA ARDHI ZANAZOMILIKIWA NA SERIKALI

Kamishna wa kaunti ya Kwale Gideon Oyagi amewaonya wakaazi wanaonuia kunyakua ardhi zinazomilikiwa na serikali akisema watakaopatikana watakabiliwa kwa mujibu wa sheria.

Akizungumza katika kaunti ndogo ya Shimba Hills kaunti ya Kwale, Oyagi amesema kwa sasa wakaazi wengi wa eneo hilo wamekuwa wakidumisha ushirikiano na serikali ya kaunti kwa kulinda ardhi zinazomilikiwa na serikali.

Oyagi amesema serikali imeweka mikakati thabiti kuhakikisha hakuna ardhi ya umma inanyakuliwa na baadhi ya watu wenye nia ya kujinufaisha kibinafsi.

Oyagi amewahimiza wawekezaji katika eneo hilo kuwekeza katika ujenzi wa nyumba jambo litakalowezesha maafisa wa usalama kupata makazi katika eneo hilo.