Meja Jenerali Juma Mwinyikai amesema operesheni linda Boni katika kaunti ya Lamu imesaidia kudhibiti usalama wa eneo la msitu wa Boni na kaunti ya Lamu kwa Jumla.
Akizungumza akiwa kaunti ya Lamu Mwinyikai amesema mikakati ambayo imewekwa na idara ya usalama nchini itasaidia katika kuboresha usalama hata zaidi.
Aidha, amesema licha ya kushuhudiwa kwa mashambulizi ya mara kwa mara katika kaunti hiyo kutoka kwa magaidi wanaoaminika kuwa wa Al –Shabaab oparesheni ya Linda Boni imesaidia kuwawezesha wenyeji kupiga hatua kimaendeleo.
Mwinyikai pia amewahakikishia wakaazi wa eneo la msitu wa Boni na kaunti ya Lamu kwa ujumla usalama wao utaendelea kuimarishwa na oparesheni ya linda Boni itaendelea hadi usalama utakapofanikishwa baada ya kuwafurusha magaidi hao wa Al – Shabaab.
OPARESHENI YA LINDA BONI KUENDELEZWA KWENYE KAUNTI YA LAMU

