NERO CHISHENGA ANAAMINI MSIMU UJAO FURUNZI ITAPATA MAFANIKIO

Mkufunzi mkuu wa kikosi cha Furunzi FC Nero Chishenga wa klabu hiyo ilopanda daraja hadi ligi ya daraja la pili kitaifa amehakikishia mashabiki kwamba wako imara kuelekea msimu ujao.

Wikendi hii klabu hiyo iliandaa harambee ya kuchangisha hela za kufadhili mechi zao msimu ujao katika uwanja wao wa furunzi uliopo mjini malindi kaunti ya Kilifi ambao Nero Chishenga anasema kwamba ulikuwa wa kufana.

Kwa sasa rabita haijatolewa rasmi ya ligi ya daraja la pili kitaifa ila kulingana na fundi huyo wa soka huenda ligi ikaanza rasmi mwezi huu wa disemba tarehe 27.

Leave a Comment

Your email address will not be published. Required fields are marked *