NAIBU WA RAIS PROFESA KITHURE KINDIKI AHUDHURIA KUAPISHWA KWA RAIS MTEULE WA TAIFA LA MOZAMBIQUE.

Naibu rais Kithure Kindiki ameondoka humu nchini mapema leo kwenda nchini Mozambique hudhuria kuapishwa kwa rais mteule nchini humo Daniel Francisco Chapo.

Naibu wa rais Kindiki anatarajiwa kuwakilisha taifa la Kenya katika hafla hiyo hatua ambayo pia itasaidia kujenga uhusiano wa taifa hili la mataifa mengine ya Afrika.

Chapo ameshinda kiti hicho kwa asilimia 65 ya kura  huku wapinzani wake na waangalizi wakidai kuwa uchaguzi huo si halali.

Matokeo hayo yamesababisha maandamano kushuhudiwa katika taifa hilo na vurugu, ambalo limesababisha kuharibiwa kwa kwa mali ya umma nchini humo.

Aidha zaidi ya watu 70 wakiwemo waandamanaji, watoto na maafisa usalama wameaga dunia tangu kuchipuka kwa hali hiyo ya ukosefu wa usalama baada ya kura hizo kupigwa mwezi October mwaka wa jana 2024.