Muungano wa maaskofu eneo la Pwani umesema kuwa ipo haja ya madhehebu ya makanisa ya taifa hili, kusajiliwa chini ya miungano mbali mbali ya makanisa humu nchini.
Wakizungumza katika kikao na wanahabari hapa mjini Malindi kaunti ya Kilifi, viongozi hao wa kidini wamesema hatua hiyo ni njia mojawapo kusaidia katika kuwachunguza baadhi ya wachungaji, ambao wamekuwa wakiendeleza mafundisho ambayo. yanapotosha waumini wa eneo la Pwani na taifa la Kenya kwa jumla.
Wakiongozwa na Askofu Abarija Kinnogah, amesema kuwa mchungaji mwenye itikadi potufu eneo la Shakahola Paul Mackenzie, hakuwa chini ya muungano wowote unaosimamaia makanisa, jambo ambalo anadai huenda likwa mojawapo ya sababu ambazo, zilichangia suala la yeye kuendeleza imani hiyo potofu.
Kauli yake imeungwa mkono na mwenyekiti wa maaskofu hao Amos Lewa pamoja na Askofu Thomas Kakhala, ambao wamesema kuwa jukumu la kuchunguza mafunzo ya wachungaji. linapaswa kukabidhiwa maaskofu hao, pamoja na viongozi wa miungano inayosimamia makanisa mbali mbali, huku wakijitenga na mchungaji wa kanisa la NEW LIFE PRAYER CENTER eneo la Mavuieni hapa kaunti ya Kilifi Ezekiel Odero.

