Mwakilishi wa kike kaunti ya Kilifi Getrude Mbeyu anamtaka waziri wa usalama wa ndani humu nchini profesa Kithure Kindiki, kuchunguzwa kuhusiana na hatua ya yeye kutokuwa na ufahamu, kuhusiana na vifo vya watu 100 katika eneo la Shakahola kaunti hii ya Kilifi.
Kulingana na Mbeyu ni kuwa waziri huyo hajaweka jitihada zaidi, katika suala la hilo ikilinganishwa na lile la wizi wa mifugo katika kaunti za Pokot na Baringo.
Katika taarifa yake kwa wanahabari, kiongozi hiyo ameeleza kugadhabishwa na suala la wanaandishi wa habari, pamoja na wanaharakati kutopewa ruhusa ya kuingia ndani ya msitu wa Shakahola, katika zoezi la kufukua miili ya baadhi ya wafuasi wa mchungaji Paul Mackenzie.
Aidha, amesisitiza kuwa ipo haja ya uchunguzi wa kina kuanzishwa dhidi ya wiziri Kindiki, kutokana na hatua hiyo.

