Muungano wa kitaifa wa watu wanaoishi na ulemavu umeikosoa serikali ya rais William Ruto kwa kile walichosema kuwa haikujumuisha watu wenye uwezo maalum katika baraza la mawaziri.
Muungano huo umesema ni wazi kuwa rais Ruto amewabagua katika baraza hilo la mawaziri huku sasa wakimtaka rais Ruto kuwazingatia katika nyadhfa zilizosalia za makatibu wakuu na makatibu wandamizi kwenye wizara mbalimbali na katika uteuzi wa uongozi wa uongozi kwenye mashirika ya kiserikali.
Wakati uo huo, muungano huo pia imekiri kuwasilisha kesi mahakamani kupinga uteuzi wa wawakilishi wadi katika kaunti 22 ambazo wanasema kuwa hazijafuata sheria katika ujumuishaji wa watu wenye uatilifu.
Joseph Atela ni mkurugenzi mkuu katika muungano huo.
Ni kauli iliyoungwa mkono na Collins Ombajo,mtetezi wa haki za watu wanaoishi na ulemavu nchini ambaye amesema kuwa kuna haja ya serikali kuzingatia haki za watu wanaoishi na ulemavu humu nchini,tamko lilipigiwa upatu na Belinda Oduor ambaye pia ni mtetezi wa haki za watu wenye uatilifu.

