MZOZO WA UONGOZI WASHUHUDIWA NDANI YA MUUNGANO WA AZIMIO LA UMOJA ONE KENYA.

Vyama tanzu vya muungano wa Azimio la Umoja One Kenya vinazozania nafasi finyu za uongozi bungeni huku kila mmoja akitaka kusitiriwa kwenye uongozi.

Mzozo wa hivi punde ni kuhusiana na utunzi wa tume inayoshughulikia maslahi ya wabunge na wafanyikazi wa bungeni ambapo mbunge wa Sirisia John Walukhe na mbunge wa Eldas Adan Keynan wanachuana kuwania wadhfa huo.

Walukhe ambaye anadaiwa kupokea uungwaji mkono kutoka kwa wenzake katika azimio la umoja one Kenya anadai kuwa Keynan anapaswa kutoa nafasi hiyo kwa kiongozi mwingine kwani amekuwa kwenye wadhfa huo kwa hatamu nne sasa. ambaye amekuwa kwenye uongozi kwa kipindi kirefu.